UFUGAJI WA MENDE:
FURSA MPYA INAYOCHANGIA UCHUMI
Ufugaji wa mende ni sekta inayokua kwa kasi hapa nchini
kutokana na faida zinazopatikana kutoka kwa wadudu hawa. Kasi hii imechochewa
na uelewa unaoendelea kuongezeka juu ya thamani ya mende katika masuala
mbalimbali kama chakula, lishe ya mifugo, na hata uzalishaji wa bidhaa za
urembo. Ufugaji wa mende hauhitaji masharti mengi wala gharama kubwa, jambo
linalowavutia wafugaji wengi kujiingiza katika biashara hii.
Kuna zaidi ya aina 400 za mende duniani, lakini aina 30
pekee hupatikana katika makazi ya binadamu. Kati ya hizi, aina 4 zinajulikana
kuwa kero katika nyumba. Hata hivyo, mende wanaofugwa kwa ajili ya chakula cha
mifugo, binadamu, na kutengeneza bidhaa za urembo ni wale waliofanyiwa mseto wa
kisayansi kwa kuchanganya mende wa Asia, Ujerumani, na Marekani. Kwa kitaalamu,
aina bora zaidi ya mende huyu anajulikana kama Diploptera punctata.
Periplaneta Americana (American Cockroach) aina hii ya mende ni maarufu
inayofugwa kwa ajili ya protini na utengenezaji wa dawa. Mende hawa wanakua
haraka na ni hodari wa kustahimili mazingira magumu, asili y amende hawa ni Afrika, lakini wameenea duniani kote.
Hupatikana sana katika maeneo ya tropiki na hali ya joto. Sifa ya mende hawa ni wakubwa kuliko aina nyingine nyingi, na
wana urefu wa hadi sentimita 5. Wana
uwezo wa kuruka, na wanapendelea mazingira yenye unyevunyevu kama vile jikoni,
mabomba ya maji, na vyooni.
Aina nyingine ni Mende wa Ujerumani (German Cockroach) na jina la kisayansi wanajulikana kama Blattella germanica, asili ya mende hawa ni Asia, lakini wameenea kote duniani, hasa katika maeneo ya mijini na sifa kubwa ya mende hawa ni ni mende wadogo wenye urefu wa takriban sentimita 1.5. Wanajulikana kuwa na uwezo wa kuzaa kwa haraka sana na wanapendelea maeneo yenye joto, hasa jikoni na vyooni.
Wako wengine
wanaojulikana Asia (Asian Cockroach) na jina la kitaalamu wanajulikana kama Blattella
asahinai na hawa asili yao ni Asia ya Kusini-Mashariki, lakini wameenea katika
maeneo mbalimbali duniani, hususan Amerika Kaskazini, sifa yao kubwa hufanana sana na mende wa Ujerumani lakini
wana uwezo mzuri zaidi wa kuruka. Wanapenda maeneo yenye mwanga kama bustani na
nje ya nyumba, tofauti na mende wengine wanaopendelea giza. Wengine ni Mende wa
Smoky Brown (Smokybrown Cockroach) jina la Kisayansi Periplaneta fuliginosa,
Mende wa Brown Banded (Supella longipalpa na aina nyingine nyingi ambayo
FAIDA ZA UFUGAJI WA MENDE
Ziko faida nyingi za ufugaji wa mende lakini faida hizi
tunaweza kuziweka katika makundi makubwa mawili ambapo ni faida za kiuchumi na
Kiafya
KIUCHUMI :
Mende hufugwa kwa gharama ndogo na kuuzwa kwa bei nzuri,
hususan kama chakula cha wanyama kama samaki na kuku. Pia, biashara ya mende
inatoa fursa kwa kupunguza taka za chakula, kwani mende wanaweza kula mabaki ya
vyakula na taka nyingine za kikaboni.
Uuzaji wa mende waliofyekwa na kukaushwa unaweza kufikia
hadi dola 20 kwa kilo moja, na hivyo kutoa faida kubwa kwa wafugaji.
KIAFYA :
• Chakula cha Binadamu: Nchini Tanzania na duniani kote,
baadhi ya watu hutumia mende kama chakula. Hasa katika nchi kama Denmark,
Brazil, na China, soko la mende kwa ajili ya chakula ni kubwa.
• Lishe ya Mifugo: Mende ni chanzo kizuri cha protini kwa
mifugo, hasa kuku. Utafiti umeonyesha kuwa mende wana kiwango kikubwa cha
protini ukilinganisha na vyakula vingine, hivyo wafugaji wengi hupendelea
kuwapa mende badala ya dagaa.
• Taaluma: Katika masomo ya biolojia, mende hutumika sana kwenye majaribio ya kisayansi. Hii inatoa fursa kwa wafugaji kuwauza mende kwa shule na taasisi za elimu kwa ajili ya majaribio.
UZALISHAJI NA UTAGAJI
Kwa kawaida, mende huchukua takriban miezi miwili na nusu kufikia umri wa kuvunwa, endapo watapatiwa chakula na maji ya kutosha. Mende wana uwezo wa kuishi hadi miaka minne, na kila mmoja ana uwezo wa kutaga kati ya mayai 55 hadi 70 mara tatu kwa mwaka. Endapo watapatiwa mazingira rafiki, asilimia kubwa ya mayai hayo hutatua na kuzalisha mende wachanga.
UJENZI WA BANDA
Banda la kufugia mende linaweza kujengwa kwa ukubwa na
muundo tofauti, kulingana na mtaji na malengo ya mfugaji. Kwa wale wanaofuga
mende kwa ajili ya chakula cha binadamu, inashauriwa kuwa na mazingira safi na
mazuri zaidi kuliko wale wanaofuga kwa ajili ya chakula cha mifugo. Zingatia
yafuatayo wakati wa kuandaa banda:
• Tengeneza mazingira yenye giza kwani mende hawapendi
mwanga.
• Hakikisha banda haliingii maji wala mwanga mwingi.
• Tumia masanduku maalumu ya mbao yenye uwezo wa kuhifadhi mende
bila kuruhusu watoke nje.
CHAKULA
Mende hula aina mbalimbali za chakula ambazo hazigharimu sana. Chakula cha mende ni rahisi na kinapatikana kwa wingi nchini, ikiwa ni pamoja na:
• Unga wa mahindi na muhogo,
• Viazi mviringo (vilivyo bora au vilivyoharibika),
• Matunda na mboga,
• Maharage yaliyopikwa na kupondwa.
Kwa kawaida, mende wanapopewa chakula cha vizuri, baada ya wiki mbili wanakuwa tayari kuvunwa wakiwa na uzito wa gramu 5, ambao ni uzito bora kwa matumizi mbalimbali.
SOKO LA MENDE
Soko la mende linaendelea kuimarika kutokana na uelewa
unaoongezeka juu ya faida za wadudu hawa. Kuna masoko kadhaa:
1. Chakula cha Binadamu: Wateja wakuu ni wachina na watu
wengine wa nje ya nchi.
2. Chakula cha Mifugo: Wafugaji wa kuku hutumia mende kama
mbadala wa dagaa.
3. Taaluma: Shule na taasisi za elimu hununua mende kwa ajili
ya majaribio ya kisayansi.
4. Wafugaji Wapya: Wafugaji wapya wanahitaji mbegu za mende kwa ajili ya kuanzisha biashara zao, hivyo kuna fursa kubwa ya kuuza mende kama mbegu.
MADHARA YA MENDE
Ingawa ufugaji wa mende una faida nyingi, kuna madhara
ambayo hujitokeza wanapokuwa kwenye makazi ya binadamu:
1. Kero: Mende huweza kusababisha usumbufu kwa kuzunguka
kwenye vyakula na vinywaji.
2. Kuchafua
Chakula: Mende hubeba vimelea vya magonjwa wanapopita kwenye chakula.
3.
Uoteshaji wa Vimelea vya Magonjwa: Baadhi ya vimelea vya magonjwa huweza kuota
ndani ya mfumo wa chakula wa mende.
4. Kuuma:
Mende wanaweza kunga'ata na kusababisha majeraha.
5. Aleji:
Mate, kinyesi, na mabaki ya mende huweza kusababisha aleji kali.
6. Uharibifu wa Vifaa vya Thamani: Mende huingia kwenye vifaa kama redio na kompyuta, na kuleta uharibifu mkubwa.
Kwa ujumla, ufugaji wa mende unatoa fursa kubwa kiuchumi na
kisayansi, na unapoendeshwa kwa ufanisi, unaweza kuwa sekta muhimu nchini.
Jiunge na chanel yetu Unique Hub channel upate taarifa na makala mbalimbali channel on WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VahNCOi4yltWEUtYCD24






0 comments: