Sunday, August 4, 2024

SOLOMON SAULI AFARIKI AJALINI




Mmiliki wa Mabasi ya Sauli afariki

Mmiliki wa mabasi ya Sauli, Bw. Solomon Sauli, amefariki dunia leo Agosti 4, 2024, majira ya saa kumi na mbili na nusu alfajiri, katika ajali ya gari iliyotokea eneo la Miwaleni, Wilaya ya Mlandizi, mkoani Pwani.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana, gari alilokuwa akisafiria Bw. Sauli lilipata hitilafu ya kiufundi na kugonga gari aina ya Jeep, kabla ya kugongana tena na gari jingine aina ya Howo linalotumika kubeba kokoto.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Bw. Pius Lutumo, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo. Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha maiti cha kituo cha afya cha Mlandizi.


 

0 comments: