Leo katika historia tunaangazia hatua za kidemokrasia kutoka USA ambapo hapo awali wanawake walikuwa hawashiriki katika zoezi la kupiga kura.
Historia ya wanawake Marekani kupata haki ya kupiga kura ni
sehemu ya harakati za muda mrefu za kutetea usawa wa kijinsia na haki za
kiraia. Harakati hizi zilianza mapema katika karne ya 19, zikiongozwa na
wanawake kama Elizabeth Cady Stanton, Susan B. Anthony, na wengine waliokuwa
sehemu ya harakati ya suffrage (haki ya kupiga kura).
Harakati hizi zilipata nguvu zaidi mnamo karne ya 20, huku
wanawake wakipigania haki yao ya kushiriki katika mchakato wa kidemokrasia.
Mwaka 1919, Congress ya Marekani ilipitisha Marekebisho ya 19 ya Katiba, ambayo
yalipendekeza kutoa haki ya kupiga kura kwa wanawake. Hata hivyo, ilibidi
marekebisho haya yaridhiwe na theluthi mbili ya majimbo kabla ya kuwa sheria.
Mnamo Agosti 18, 1920, Tennessee ikawa jimbo la mwisho kati
ya 36 zilizohitajika kuridhia marekebisho haya, na hivyo Marekebisho ya 19
yakawa sehemu ya Katiba ya Marekani. Hii iliwapatia wanawake haki ya kupiga
kura kwa mujibu wa sheria za kitaifa.
Marekebisho ya 19 yaliridhiwa chini ya uongozi wa Rais Woodrow
Wilson, ambaye alihudumu kama Rais wa Marekani kutoka 1913 hadi 1921. Ingawa
hapo awali Wilson alikuwa na mawazo tofauti kuhusu haki za wanawake, shinikizo
la harakati za wanawake na mabadiliko ya kisiasa ulimlazimu kutoa msaada wake
kwa marekebisho haya muhimu.
Endelea kutufuatilia kwa makala mbalimbali na habari kupitia https://geomondy.blogspot.com
Na unaweza kujiunga na channeli yetu whatsaap https://whatsapp.com/channel/0029Va96t2m5PO13ZnTUCL3i

0 comments: