Kamala Harris Ahamasisha Uungwaji Mkono wa Wanawake Weusi
katika Mabadiliko ya Kampeni za Kidemokrasia
Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris, aliwahutubia zaidi ya wanawake 6,000 weusi katika mkutano wa kisiasa mjini Indianapolis, Julai 24. Harris aliwataka wanawake hao kusaidia kuimarisha kampeni za urais za Kidemokrasia baada ya Rais Joe Biden kujiondoa kwenye kinyang'anyiro.
Harris alisisitiza umuhimu wa wanawake weusi katika historia ya siasa na kuwasihi waunge mkono chama cha Kidemokrasia. Wito huu unakuja wakati mpinzani wake wa Republican, Donald Trump, akijiandaa kurejea kwenye kampeni.
Kwa uongozi wa Harris, kampeni za Kidemokrasia zina nguvu mpya, huku akilenga kuimarisha uungwaji mkono na kukabiliana na kasi ya Trump. Uchaguzi wa Novemba 5 unatarajiwa kuwa na ushindani mkali.
Harris anachukua nafasi baada ya Joe Biden kujiondoa kwenye
kinyang'anyiro hicho na kumpendekeza mwanamama Harris kuwa mgombea wa urais
kupitia chama cha Kidemokrasia.

0 comments: