Friday, July 19, 2024

RUTO ATOA ORODHA YA MAJINA 11 WATEULE KWA NAFASI YA BARAZA LA MAWAZIRI.

 

Rais wa Kenya William Ruto jana 19 Julai ametoa orodha ya majina 11 ya wateule kwa nafasi za baraza la mawaziri, ikiwemo nafasi ya Mwanasheria Mkuu. Wateule hawa wanasubiri kuidhinishwa na Bunge la Kenya. Hatua hii inafuatia kuvunjwa kwa baraza la mawaziri la awali kutokana na shinikizo la wananchi kutaka mabadiliko ya serikali. Walioteuliwa ni:


1. Wizara ya Mambo ya Ndani na Utawala wa Kitaifa - Kithure Kindiki

2. Wizara ya Afya - Debra Mulongo Barasa

3. Wizara ya Ulinzi - Aden Duale

4. Wizara ya Barabara na Uchukuzi - Davis Chirchir

5. Wizara ya Mazingira, Mabadiliko ya Tabia nchi na Misitu - Soipan Tuya

6. Wizara ya Maji, Usafi wa Mazingira na Umwagiliaji - Eric Muga

7. Wizara ya Elimu - Julius Migosi

8. Wizara ya Kilimo na Maendeleo ya Mifugo - Andrew Muhia Karanja

9. Wizara ya Ardhi, Kazi za Umma, Nyumba na Maendeleo ya Miji - Alice Wahome

10. Mwanasheria Mkuu - Rebecca Miano


Rais Ruto alitangaza wateule hao katika hotuba kwa taifa pamoja na mabadiliko hayo bado kuna dalili ya kuwepo kwa upinzani toka kwenye kundi la GEN Z ambao wanaonesha kuendelea na dhamira yao.

0 comments: