Wednesday, July 31, 2024

SGR YAZIMIKA TRC YAOMBA RADHI


 TRC Yaomba Radhi kwa Hitilafu ya Umeme Iliyosababishwa na wanyama

Shirika la Reli Tanzania (TRC) limeomba radhi baada ya hitilafu ya umeme kutokea kati ya stesheni ya Kilosa na Kidete, kusababisha kusimama kwa muda wa saa mbili kwa treni ya reli ya kiwango cha kimataifa (SGR) iliyokuwa ikisafiri kutoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma mnamo Julai 30, 2024. TRC imesema hitilafu hiyo ilisababishwa na wanyama kama ngedere au bundi kugusa nyaya za reli. Mafundi walitatua tatizo na kurejesha umeme saa 6:30 usiku, na treni iliendelea na safari, kuwasili Dodoma saa 7:57 usiku.

0 comments: