Friday, July 19, 2024

RC MAKONDA AKUTWA NA HATIA


THBUB Yabaini Matumizi Mabaya ya Madaraka na Paul Makonda

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imemkuta na hatia Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, kwa matumizi mabaya ya madaraka. Makonda aliamuru kukamatwa kwa mwananchi mmoja na kuwekwa rumande kwa saa 96 bila kufunguliwa mashtaka.

Akizungumza jana Ijumaa, Julai 19, 2024, jijini Dodoma, Mwenyekiti wa THBUB, Jaji mstaafu Mathew Mwaimu, alisema Makonda alikaidi kuitwa mbele ya tume kuwasilisha utetezi wake. Taarifa hiyo ilitolewa wakati wa kupokea na kuchunguza malalamiko ya ukiukwaji wa haki za binadamu na utawala bora kwa mwaka 2022/23.

Tume ilibaini kuwa amri ya Makonda haikuwa halali na ilikiuka taratibu za kisheria. Mwananchi huyo hakuwa na hatia yoyote katika madai yaliyotolewa. Jaji Mwaimu alisema Makonda alivuka mipaka ya majukumu yake kwa kushughulikia suala lililopaswa kushughulikiwa kisheria.

Jitihada za kumtafuta Makonda kwa simu yake ya mkononi hazikufanikiwa. Katika kipindi cha mwaka 2022/23, THBUB ilipokea malalamiko 1,524 na kumaliza 789, huku 885 yakiendelea kufuatiliwa

0 comments: